mapenzi app

Maumivu wakati wa kufika kileleni kwa Mwanaume






FAHAMU TIBA YA MAUMIVU WAKATI WA KUFIKA KILELENI KWA MWANAUME.

PAINFUL EJACULATION/PAINFUL ORGANS IN MALE.
Ni ile hali ya mwanaume kuhisi maumivu wakati anafika kileleni/wakati manii yanatoka au mda mfupi baada ya kufika kileleni.
Maumivu hayo anaweza kuyahisi Perinium(eneokatikati ya tundu la choo kubwa au korodani au yanaweza yakawa kwenye mrija ambao unatiririsha manii pake mwanaume anapofika kileleni na unatiririsha mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo hadi nje ya mwili.
Hii hali huwaga inawanyima raha wanaume wengi wanajikuta hata hawafurahii tendo la ndoa.
Sababu kubwa ya maumivu haya wakati wa kufika kileleni mwanaume ni kama ifuatavyo:-
1. Kuvimba kwa korodani tezi dume au urethra au njia inayotiririsha manii kutoka kwenye tezi dume kwenda nje ya mwili, uvimbe huu unaweza ukasababishwa na kushambuliwa kwa hizo sehemu na vimelea vya iana mbali mbali mf.
2. Magonjwa ya zinaa ni chanzo kingine kama, ( kisonono, kaswende, pangusa n mengine)
3. Kuharibika kwa mishipa ya fahamu (Nerve) ambayo inasaidia usimamaji wa uume. Kwahiyo wakati wa kufika kileleni misuli ya uume huaga inajikamua ili kusukuma Manii nje kunaweza kutonesha ile sehemu ambapo nerve imeathirika.
4. Kuziba kwa mrija unaotiririsha Manii unaweza kusababisha maumivu wakati wa kufika kileleni
5. Kansa ya tezidume(PROSTATE CANCER) ni chanzo kingine
6. Kufanyiwa upasuaji /opaeration inayohusu viungo vya uzazikunaweza kukusababisha maumiv pale endapo mwanaume atashiriki tendo la ndoa kabla ya kupona vizuri.
7. Maumiv ya nyonga mara kwa mara yanaweza yakasababisha pia maumiv wakati wa kufika kileleni.
8. Matatizo ya kisaikolojia pia ni chanzo kingine cha haya maumivu.

DALILI
1.Maumivu ya wakati wa kufika kileleni ni dalili kuu lakini kuna dalili ambazo zina ambatana na dalili hiyoamabazo nii maumiv ya kiuno, nyonga, korodani,na maumivu chini ya kitovu ni dalili nyingine.
MATIBABU
Matibabu ya hili tatizo yanategemea chanzo cha tatizo, ambapo chanzo chanzo cha tatizo kinabainika baada ya kipimo,

MADHARA ENDAPO MGONJWA HATATIBIWA MAPEMA.
i. Kushindwa kuridhishana baina ya wapenzi katika tendo la ndoa
ii. Mwanaume anaweza akashindwa kujiamini
iii. Kukosa hisia ya kushiriki tendo la ndoa
iv. Upungufu wa nguvu za kiume, kwa maana ya uume kusimama legelege, kuwahi kufika kileleni na kutokua na uwezo wa kurudia tendo baada ya kufika kileleni.

USIPITWE NA HABARI,MATUKIO,SIMULIZI KALI ZA MAPENZI,MIKASA,MAFUNDISHO KUHUSU MAPENZI KILA SIKU BOFYA HAPA KUDOWNLOAD APP YETU SASA NI BURE KABISA

mapenzi app

My name is mapenzi app

weka email yako hapa tukutumie habari kila siku :